|
NA MWANDISHI WETU
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimesema bado kina imani na Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya. Imesema licha ya CCM kutofautiana kimawazo katika baadhi ya maeneo katika rasimu ya kwanza ya katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini haina ugomvi na tume hiyo. Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. "Tunawaheshimu sana wajumbe wa tume hii, na kwa kweli tunamatumaini nao sana kuwa watatimiza wajibu wao kwa weledi mkubwa", alisema Nape. Nape alibainisha kwamba pamoja na maeneo mengine ya rasimu ya kwanza ya katiba , CCM ina mawazo tofauti kwenye suala la Muundo wa Muungano ambapo wakati rasimu inapendekeza muundo wa serikali tatu, CCM yenyewe inapendekeza serikali mbili. "Kama mnavyoona katika hili, wakati tume inapendekeza muundo wa serikali tatu sisi CCM tunapendekeza muundo wa serikali mbili, lakini hii haitufanyi tuwapuuze au tugombane na wale wenye mawazo tofauti na yetu", alisema Nape na kuongeza; "Kumekuwepo na ripoti na makala kadhaa zinazojaribu kuonyesha kama vile kuna mvutano kati ya tume na CCM, au CCM na wengine wenye mawazo tofauti na CCM. Ukweli ni kuwa hali hiyo inayojaribu kujengwa kwa nguvu si ya kweli. Tuache hoja zishindane kwa hoja na nguvu ya hoja ndio iwe msingi wa ushindani". Nape alitaka ushindani uwe kwenye hoja bila kushutumiana ili jatimaye mawazo ya wengi yasikilizwe na kuzingatiwa. Alisema, CCM inasisitiza kuwa itaheshimu mawazo ya Watanzania, kwani katiba inayotengenezwa ni ya watanzania wote bila ya kujali itikadi zao. "Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote wanaounga mkono baadhi ya hoja za CCM hasa hoja ya serikali mbili. Tumeshuhudia maoni ya wajumbe wengi wa mabaraza na wananchi kwa ujumla wakiunga mkono mawazo haya ya CCM ya muundo wa muungano wa serikali mbili na hoja kadhaa zingine", alisema Nape na kuongeza; "CCM tunapenda kuwashukuru wote. Tujadili kwa kuvumiliana, tukipendana na kuheshimiana. Tanzania yenye neema tele inawezekana". |
WAPINZANI WACHEZEA KICHAPO KIBONDO |
Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chamilion wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.Diwani wa CCM Ndugu Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.Kabla ya uchaguzi huo palikuwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani wa CCM, mgogoro ambao ulitatuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye kufuatia ziara yake ya kimyakimya ya siku moja wilayani Kibondo ambapo alikutana na madiwani hao wa CCM kwa zaidi ya masaa manne.Matokeo haya ni kinyume kabisa na kile kilichoandikwa na Gazeti la Tanzania Daima la Agosti 7,2013 kuwa ' WIKI NGUMU KWA CCM" wakieleza kuwa CCM wangepoteza uchaguzi huu. Fitina hiyo ya TanzaniaDaima imegeuka kuwa bahati kwa CCM maana imetembeza kichapo cha haja kwenye uchaguzi huo.Nape akiongea juu ya ushindi huo akinukuliwa na redio moja ya Mjini Mwanza alisema "ushindi huo ni mawingu mvua zenyewe zinakuja. Unajua hawa jamaa wanawekeza kwenye migogoro ndani ya CCM ili ikitokea hatukuelewana mahali basi wanazamia, hapa nimewazidi akili" alikaririwa Nape. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni