Jumapili, 11 Agosti 2013

MAN UNITED v/s WIGAN ATHLETIC NGAO YA HISANI WEMBLEY

MAN UNITED WAICHAPA WIGAN ATHLETIC NA KUTWAA NGAO YA HISANI WEMBLEY


 



 Umati wa mashabiki wa soka ukiwa unaingia ndani ya Uwanja wa Wembley jijini London, kuangalia pambano la Ngao ya Hisani kati ya Manchester United na Wigan Athletic, ambapo United imeshinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Robin van Persie (Picha kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza)
 
Man United (kulia) nma Wigan (kushoto), wakiwa wamejipanga kabla ya kuanza kwa pambano la Ngao ya Hisani kwenye dimba la Wembley jijini London. Mechi hiyo inayohusisha mabingwa wa Ligi Kuu na wale wa Kombe la FA, ni kiashiria cha ufunguzi wa msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu ya England.
On form: Van Persie scored a double as Manchester United beat Wigan 2-0 at Wembley
Kwenye kiwango cha juu: Robin Van Persie aliifungia Man United mabao yote mawili (moja kila kipindi), kuipa timu yake ubingwa wa Ngao ya Hisani na ushindi wa kwanza kwa kocha mpya David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
Early blow: Robin van Persie headed Manchester United into the lead in the sixth minute
Bao la mapema: Robin van Persie akijitisha mpira kufunga kwa kichwa, kuipa Manchester United bao la uongozi katika dakika ya sita ya pambano holo Wembley.
In action: Manchester United's Atonio Valencia takes the ball away from Wigan's Jordi Gomez
Kikazi zaidi: Winga wa Manchester United, Atonio Valencia akimtoka beki wa Wigan, Jordi Gomez.
Ahead: The Dutchman arrived late in the penalty area to head Patrice Evra's cross into the bottom corner
Joy: United celebrate Van Persie's early goal at Wembley
Raha ya ushindi: Nyota wa Man United wakishangilia bao la mapema la Van Persie kwenye dimba la Wembley.
New signings: United's Wilfried Zaha, (left) competes with Wigan Athletic's James McClean
Usajili mpya Old Trafford: Nyota mpya wa Man United, Wilfried Zaha, (kushoto) akichuana na mchezaji wa Wigan Athletic, James McClean.
Elusive: United's new winger Wilfried Zaha escapes the attention of Ben Watson
Nakutoka hivi: Winga mpya wa Man United, Wilfried Zaha akichanja mbuga kumtoka Ben Watson.
Vocal: David Moyes and Owen Coyle shout out instructions to their teams
Maelekezo ya makocha: David Moyes wa Man United (kushoto) na Owen Coyle wa Wigan Athletic, wakitoa maelekezo kwa wachezaji wao.
Advantage doubled: Van Persie net's Manchester United's second goal just before the hour mark
Natikisa hivi nyavu: Van Persie akiifungia Manchester United bao la pili kuipa ushindi wa mabao 2-0.
Challenge: Manchester United's Nemanja Vidic comes under pressure from Shaun Maloney
Mchuano dimbani: Beki wa Manchester United, Nemanja Vidic akichuana na Shaun Maloney wa Wigan Athletic.
Race: Chris Smalling (left) competes with McClean to reach the ball
Mbio dimbani: Beki Chris Smalling (kushoto) wa Man United, akishindana mbio kuwania mpira na McClean wa Wigan Athletic.
The heat is on: Manchester United and Wigan walk out onto the pitch at Wembley
From the front: Manchester United manager Moyes leads his team out at Wembley
Bosi kazini: Kocha mpya wa Manchester United, Moyes akiongoza nyota wa kikosi chake katika mechi hiyo.
New toy: Fourth official Michael Oliver tests out the Goal Decision System before the match
Majaribio GLT: Mwamuzi wa akiba, Michael Oliver akifanyia majaribio mfumo mpya wa Goal Line Technology (GLT), ulioanza kutumiwa katika mechi hiyo ya Ngao ya Hisani na kutarajiwa kutumiwa katika Ligi Kuu ya England.
Iconic walk: Fans make their way down Wembley Way for the Community Shield
Twenzetu!!! Mashabiki wakiingia Uwanja wa Wembley

Jumamosi, 10 Agosti 2013

CCM NA MABADILIKO YA KATIBA


NA MWANDISHI WETU
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimesema bado kina imani na Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya.

Imesema licha ya CCM kutofautiana kimawazo katika baadhi ya maeneo katika rasimu ya kwanza ya  katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini haina ugomvi na tume hiyo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

 "Tunawaheshimu sana wajumbe wa tume hii, na kwa kweli tunamatumaini nao sana kuwa watatimiza wajibu wao kwa weledi mkubwa", alisema Nape.

Nape alibainisha kwamba  pamoja na maeneo mengine ya rasimu ya kwanza ya katiba ,  CCM ina mawazo tofauti kwenye suala la Muundo wa Muungano ambapo wakati rasimu inapendekeza muundo wa serikali tatu, CCM yenyewe inapendekeza  serikali mbili.

"Kama mnavyoona katika hili, wakati tume inapendekeza muundo wa serikali tatu sisi CCM tunapendekeza muundo wa serikali mbili, lakini hii haitufanyi tuwapuuze au tugombane na wale wenye mawazo tofauti na yetu", alisema Nape na kuongeza;

"Kumekuwepo na ripoti na makala kadhaa zinazojaribu kuonyesha kama vile kuna mvutano kati ya tume na CCM, au CCM na wengine wenye mawazo tofauti na CCM. Ukweli ni kuwa hali hiyo inayojaribu kujengwa kwa nguvu si ya kweli. Tuache hoja zishindane kwa hoja na nguvu ya hoja ndio iwe msingi wa ushindani".

Nape alitaka ushindani uwe kwenye hoja bila kushutumiana ili jatimaye mawazo ya wengi yasikilizwe na kuzingatiwa.

Alisema, CCM inasisitiza kuwa itaheshimu mawazo ya Watanzania, kwani katiba inayotengenezwa ni ya watanzania wote bila ya kujali itikadi zao.

"Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote wanaounga mkono baadhi ya hoja za CCM hasa hoja ya serikali mbili. Tumeshuhudia maoni ya wajumbe wengi wa  mabaraza na wananchi kwa ujumla wakiunga mkono mawazo haya ya CCM ya muundo wa muungano wa serikali mbili na hoja kadhaa zingine", alisema Nape na kuongeza;

"CCM tunapenda kuwashukuru wote. Tujadili kwa kuvumiliana, tukipendana na kuheshimiana. Tanzania yenye neema tele inawezekana
".

WAPINZANI WACHEZEA KICHAPO KIBONDO



Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chamilion wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.

Diwani wa CCM Ndugu  Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.

Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.

Kabla ya uchaguzi huo palikuwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani wa CCM, mgogoro ambao ulitatuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye kufuatia ziara yake ya kimyakimya ya siku moja wilayani Kibondo ambapo alikutana na madiwani hao wa CCM kwa zaidi ya masaa manne.

Matokeo haya ni kinyume kabisa na kile kilichoandikwa na Gazeti la Tanzania Daima la Agosti 7,2013 kuwa ' WIKI NGUMU KWA CCM" wakieleza kuwa CCM wangepoteza uchaguzi huu. Fitina hiyo ya TanzaniaDaima imegeuka kuwa bahati kwa CCM maana imetembeza kichapo cha haja kwenye uchaguzi huo.

Nape akiongea juu ya ushindi huo akinukuliwa na redio moja ya Mjini Mwanza alisema "ushindi huo ni mawingu mvua zenyewe zinakuja. Unajua hawa jamaa wanawekeza kwenye migogoro ndani ya CCM ili ikitokea hatukuelewana mahali basi wanazamia, hapa nimewazidi akili" alikaririwa Nape.