MAN UNITED WAICHAPA WIGAN ATHLETIC NA KUTWAA NGAO YA HISANI WEMBLEY

Umati
wa mashabiki wa soka ukiwa unaingia ndani ya Uwanja wa Wembley jijini
London, kuangalia pambano la Ngao ya Hisani kati ya Manchester United na
Wigan Athletic, ambapo United imeshinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na
Robin van Persie (Picha kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza)
Man
United (kulia) nma Wigan (kushoto), wakiwa wamejipanga kabla ya kuanza
kwa pambano la Ngao ya Hisani kwenye dimba la Wembley jijini London.
Mechi hiyo inayohusisha mabingwa wa Ligi Kuu na wale wa Kombe la FA, ni
kiashiria cha ufunguzi wa msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu ya England.
Kwenye
kiwango cha juu: Robin Van Persie aliifungia Man United mabao yote
mawili (moja kila kipindi), kuipa timu yake ubingwa wa Ngao ya Hisani na
ushindi wa kwanza kwa kocha mpya David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir
Alex Ferguson.
Bao
la mapema: Robin van Persie akijitisha mpira kufunga kwa kichwa, kuipa
Manchester United bao la uongozi katika dakika ya sita ya pambano holo
Wembley.
Kikazi zaidi: Winga wa Manchester United, Atonio Valencia akimtoka beki wa Wigan, Jordi Gomez.
Raha ya ushindi: Nyota wa Man United wakishangilia bao la mapema la Van Persie kwenye dimba la Wembley.
Usajili
mpya Old Trafford: Nyota mpya wa Man United, Wilfried Zaha, (kushoto)
akichuana na mchezaji wa Wigan Athletic, James McClean.
Nakutoka hivi: Winga mpya wa Man United, Wilfried Zaha akichanja mbuga kumtoka Ben Watson.
Maelekezo ya makocha: David Moyes wa Man United (kushoto) na Owen Coyle wa Wigan Athletic, wakitoa maelekezo kwa wachezaji wao.
Natikisa hivi nyavu: Van Persie akiifungia Manchester United bao la pili kuipa ushindi wa mabao 2-0.
Mchuano dimbani: Beki wa Manchester United, Nemanja Vidic akichuana na Shaun Maloney wa Wigan Athletic.
Mbio dimbani: Beki Chris Smalling (kushoto) wa Man United, akishindana mbio kuwania mpira na McClean wa Wigan Athletic.
Bosi kazini: Kocha mpya wa Manchester United, Moyes akiongoza nyota wa kikosi chake katika mechi hiyo.
Majaribio
GLT: Mwamuzi wa akiba, Michael Oliver akifanyia majaribio mfumo mpya wa
Goal Line Technology (GLT), ulioanza kutumiwa katika mechi hiyo ya Ngao
ya Hisani na kutarajiwa kutumiwa katika Ligi Kuu ya England.
Twenzetu!!! Mashabiki wakiingia Uwanja wa Wembley

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni