NA BASHIR
NKOROMO
WALIOBOBEA
katika medani ya falsafa husema, adui yako siyo lazima awe yule anayekunyooshea
silaha ili kudhuru mwili au maisha yako, bali hata asiyekutakia mafanikio mema
na kupuuza harakati zako za kimaendeleo ni adui tena namba moja.
Kwa mujibu wa
wanafalsafa hao, tofauti na adui wa kukudhuru mwili au maisha yako ambaye
akikushikia silaha unamtambua mara moja, asiyekutakia mema na kupuuza harakati
zako za kimaendeleo, inakubidi uwe mweledi sana kumtambua haraka.
Wanasema, moja
ya dalili za adui wa aina hiyo, ni yule ambaye ukifanya jambo linalokupeleka kwenye
mafanikio makubwa analiponda kuwa halifai, na ukifanya baya linalokudidimiza
anakusifia kwamba hilo ndilo zuri na la maana kuendelea nalo.
Ushauri
unaotolewa na wanafalsafa hao, ni kwamba, ukishamtambua mtu kuwa ni adui yako,
ukimsikia anakusifu kuwa jambo fulani unalofanya ni nzuri achana nalo mara
moja, lakini akiliponda kwa nguvu zake zote kuwa unalofanya halina manufaa na
kwamba ni la hovyo sana, basi jambo hilo ni jema, endelea kulifanya, yaani
songa nalo mbele.
Katika gazeti
moja la Raia Mwema, ambalo nimetokea kuliamini sana kuwa ni moja ya magazeti
mahiri nchini na bila shaka nitaendelea kuamini hivyo, katika toleo lake la
Novemba 28, mwaka huu, Mwandishi mmoja Evarist Chahali ambaye ameandika
uchambuzi wake akiwa Uskochi, amejaribu kuandika uchambuzi alioupa kichwa
cha 'Kosa la Kwanza kwa Kinana'.
Katika
mtiririko wa uchambuzi huo ameeleza mengi akimsadifu Kinana hadi na wanasiasa
za Marekani. Lakini kwa kuwa sina muda na nafasi ya kutosha ya kukuchosha
msomaji kwa kuyarejea aliyoandika, afadhali nijadili naye kuhusu jambo moja tu
alilojaribu kulifanya jamii ilione kuwa ni kosa la kwanza alilofanya Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, wakati wa mkutano wa CCM, uliofanyika mjini
Geita wiki iliyopita.
Chahali
anajaribu kushawishi wasomaji wakubaliane nake kwamba hatua ya Kinana kukabidhi
leseni kwa wachimbaji madini wadogo 21, kwenye machimbo ya Mugusu, wakati wa
mkutano huo eti ilikuwa ni aina ya kuhodhi mamlaka ya Wizara ya Nishati na
Madini inayoratibu na kusimamia shughuli za madini nchini ikiwemo uchimbaji.
Tena anaenda
mbali zaidi kwamba, kwa Kinana kufanya hivyo, inaweza kutafsirika kuwa ni
mwendelezo wa vitendo vya kifisadi kwenye sekta ya madini hapa nchini, akisema
kwamba huenda waliokabidhiwa leseni zile siyo wamiliki halisi wa leseni hizo,
kwamba ni mamluki waliozipokea leseni hizo wakiwa ni vivuli vya watu wengine.
Pangine, hili
la uwezekano wa kwamba waliopewa leseni walikuwa vivuli vya wengine,
nisilisemee sana, kwa kuwa inawezekana. Lakini ili kulithibitisha hilo ni
lazima anayetuhumu hivyo ajiridhishe kwa kujiuliza kwamba inawezekanaje hao
wachimbaji wadogo 21, wawe mazuzu kiasi cha kushangilia kuzipokea leseni hizo
wakati wanajua siyo zao, hasa ikizingatiwa kwamba hao ni miongoni mwa wakazi wa
Geita ambao kilio chao cha kila siku ni kupata leseni za uchimbaji mdogo kwenye
eneo hilo la Mgusu?
Na kama pengine
walilipwa ili kuzipokea, mamia ya watu waliokuwa kwenye mkutano ule nao
walishawishika vipi hadi nao wakashangilia hatua hiyo badala ya kuzomea? Maana
waliokuwa kwenye mkutano huo wanawajua wote waliopakabidhiwa leseni hizo kwa
sababu wote ni wakazi wa Geita.
Mimi ni
miongoni mwa mamia ya watu waliokuwa kwenye mkutano huo wa hadhara wa CCM
ambao Kinana akikabidhi leseni hizo.
Ni kwamba,
Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa imeshapitia taratibu zote za kutoa leseni
hizo, na kilichofanyika pale ni tukio la kukabidhi leseni tu, kama vile Mkuu
shule ya Sekondari, Chuo cha Ufundi au Chuo Kikuu, ambavyo huandaa vyeti
kwa ajili ya wahitimu kisha kazi ya kuwakabidhi wanaostahili ikafanywa na mgeni
rasmi aliyealikwa kwenye mahafali.
Hivi Chahali na
wengine wenye mtazamo kama yeye (kama wapo), kama mgeni rasmi akikabidhi hivyo
vyeti kwa wahitimu waliostahili kwa kufuzu kwa vigezo, ndiyo inamaanisha kwamba
amepora mamlaka ya shule au chuo husika?
Maana katika
mkutano ule, ambao bila shaka asiye itakia mema CCM ulimkera, Watendaji wa
Wizara ya Nishati na Madini, kama Taasisi ya serikali inayotekeleza ilani ya
Chama Cha Mapinduzi kilichopewa na wanachi ridhaa ya kuunda serikali,
walikuwepo kutokana na kuitwa na mwajiri wao CCM ili kueleza wanavyosimamia kwa
manufaa ya umma sekta ya madini.
Ili waweze
kueleza vizuri mbele ya wananchi, ilikuwa ni lazima waje na ushahidi wa kutosha
kuwaridhisha wananchi hao na mwajiri mwenyewe (CCM) juu ya usimamizi huo katika
rasilimali hiyo adhimu Tanzania.
Chama Cha
Mapinduzi ambacho ndicho chenye mkataba na wananchi tangu uchaguzi mkuu
uliopita, kilikuwa tayari kina malalamiko kwamba wakazi wa Geita wanapata dhiki
kutokana na kutopewa fursa ya kuruhusiwa kufanya uchimbaji mdogo katika mgodi
wa Mugusu.
Sasa kwenye
mkutano akaja Naibu Waziri wa Nishati na madini anayeshughulikia madini, Steven
Masele. Alifika kuitika wito wa CCM yaani mwajiri wa serikali iliyopo
madarakani, Kinana, kisha akapandishwa jukwaani akahojiwa mbele ya
wananchi, Je bwana mmefikia wapi katika kutatua kero hii ya wachimbaji wadogo?
Masele akajibu " Tunazo leseni 21 kwa ajili ya wachimbaji wadogo
waliofaulu vigezo ambazo tunaweza kuwakabidhi wakati wowote.
Kinana
akamuuliza Masele " Je, leseni hizo zimepitia utaratibu wote vizuri na
zipo tayari kuweza kukabidhiwa kwa hao wachimbaji? Masele akajibu,
"ndiyo".
Baada ya hapo
Naibu Waziri akamuomba Kinana kuwakabidhi leseni zao wahusika. Kinana akafanya
kazi hiyo ikakamilika bila malalamiko, maana ilifuatiwa na nderemo na vifijo
kwa waliopewa leseni hizo na pia kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Kimsingi
mtiririko mzima wa kukabidhi hati hizo ulikuwa hivyo, lakini cha kushangaza ni
kwamba mchambuzi wa makala hiyo, Chahali amejaribu, kutengeneza mawazo
yananyowafanya baadhi ya wasomaji wake wadhanie leseni zile zilitolewa ghafla,
papo hapo na CCM!
Bila shaka
Chahali amebahatika kusoma na kuhitimu masomo yake, na bila shaka wakati wa
mahafali alikabidhiwa cheti na mgeni rasmi, siyo Mkuu wa Chuo. Je, wakati
anapokea cheti hicho alisita kwa kuhofia kwamba kwa mgeni rasmi kumkabidhi
cheti hicho alikuwa anapora mamlaka ya mkuu wa chuo?
La msingi hapa
ni kwamba, hatua ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kuwakabidhi leseni
wachimbaji hao wadogo halikuwa na ukiukwaji wowote na lilikuwa jema kwa CCM,
ndiyo sababu kalamu za wasioitakia mema CCM wanaotamani wakiamka wakute
imeondoka madarakani zimekemea tena kwa ukurasa mzima kwamba lilikuwa tukio
baya na kosa la kwanza kwa katibu Mkuu huyo.
Kwa mtazamo
wangu na kwa kuzingatia ushauri wa wanafalsafa, Kinana usiungame kwamba
ulilofanya ni kosa la kwanza, isipokuwa ni moja ya matukio bora ya kwanza
uliyofanya katika ziara yako ya kwanza tangu uteuliwe kuwa Katibu Mkuu wa CCM
mapema mwezi huu kule mjini Dodoma.
Songa mbele,
huku ukijitahidi kutojaribu kufanya hata moja ambalo hao wasioitakia mema CCM
(ambao kwa dalili zao unawajua) watakusifu. Na siku ukiteleza ukalifanya jambo
ukasikia wamekusifu hadharani, lichunguze kwa makini na uliache mara moja,
usiendelee nalo.
Posted by CCM Blog

|